HabariNews

Wakaazi wa Owino Uhuru kaunti ya Mombasa watishia kuandamana kutokana na kucheleweshwa kwa fidia yao.

Licha ya mahakama kuamuru wakaazi wa Owino Uhuru kaunti ya Mombasa kulipwa fidia ya shilingi bilioni 2 mwaka jana kutokana na athari za madini ya risasi bado hawajapokea fidia hiyo.
Wakaazi hao wametishia kuandaa maandamano iwapo hapatakuwa na mabadiliko katika kesi hiyo huku wakiwataka waliokataa rufaa kufika mahakamani
Baadhi ya wakaazi wamepoteza maisha yao na wengine kulemaa kutokana na athari za madini hayo huku waathiriwa wanasema kuwa wanapata shida kupata dawa za kutumia kwani utoaji wa dawa katika hospitali ya Port Reitz ulisitishwa.

BY EDITORIAL DESK