AfyaHabariNews

Wahudumu wa afya kaunti ya Kwale watishia kugoma kuanzia kesho.

Shughuli za matibabu katika hospitali za umma kaunti ya Kwale zitatazika kuanzia kesho iwapo wahudumu wa afya watasusia kazi kama walivyotangaza.
Wahudumu hao wa afya walitoa makataa ya siku saba kwa serikali ya kaunti ya Kwale kutekeleza mkataba wa makubaliano wa mwaka 2013 huku muda huo ukikamilika hii leo.
Wakiongozwa na mwakilishi wa muungano wa wauguzi tawi la Kwale Mary Kache, wanasema kati ya masuala wanayotaka kuangaziwa ni kucheleweshwa kwa marupurupu yao kwa muda wa takriban miaka 2 pamoja na kucheleweshwa kupandishwa vyeo.

BY EDITORIAL DESK