HabariSiasa

Vigogo wa muungano wa One kenya alliance wamefanya mazungumzo ya Kina na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.

Vigogo wa muungano wa One kenya alliance Oka kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper na mwenzake Gideon Moi wa KANU wamefanya mazungumzo ya Kina na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika Ikulu ya Nakasero Jijini Kampala.
Museveni, Kalonzo na Moi, wamelifanya Kipaumbele swala la hali ya kitaifa nchini Sudan Kusini, vile vile mipango ya mwisho ya upatanisho baina ya Rais Salva Kiir, na makamo wake na Riek machar.

Vile vile Swala la uhusiano baina ya kenya na Uganda limetiwa kipaumbele wakati wa mazungumzo hayo.

Awali kalonzo alikuwa amefanya mazungumzo na aliyekuwa Balozi wa Uganda Nchini Sudan Kusini Betty Bigombe, Vile vile Balozi wa Uingereza nchini Uganda katika hoteli moja jijini Kampala.

Mazungumzo hayo aidha yalijikita Zaidi katika maswala ya usalama ya kikanda na mgogoro nchini Sudan Kusini.

BY EDITORIAL DESK