HabariNewsSiasa

Hussein Dado asema hatakubali njama ya kumshawishi kujitoa katika kinyang’anyiro cha ugavana wa Tana river.

Aliyekuwa naibu waziri katika wizara ya usalama wa ndani Hussein Dado amesema hatakubali njama ya kumshawishi kujitoa katika kinyang’anyiro cha ugavana wa Tana river na asalie katika cheo chake cha kitaifa.
Dado anasema njama hizo hazitafaulu kwani ameamua kupigania ugavana kupitia chama cha jubilee huku akisema hatakubali watu wachache kutoka nje ya kaunti hiyo kuingilia siasa za tanariver.
Dado ambae amewahi kuhudumu kama gavana wa kwanza wa tanariver amekita kambi mjini bura ambayo ni ngome ya mpinzani wake Ali Wario mbunge wa eneo hilo

BY EDITORIAL DESK