HabariNews

Khadija Binti Mzee apokea tuzo ya mwanahabari bora wa mwaka kutoka Muslims for Human Rights (MUHURI).

Mtangazaji wa Kipindi cha sauti ya mwanamke hapa Sauti ya Pwani Khadija Binti Mzee ameteuliwa miongoni mwa wanaowania tuzo za wanahabari wanaochangia maendeleo na kupigania swala la ukeketaji wa wanawake.Binti Mzee ambaye amewahi kunyakuwa tuzo mbali mbali za utangazaji hapa nchini amekuwa mstari wa mbele kuangazia manufaa na hata changamoto wanazopitia wanawake katika jamii ya sasa katika kipindi chake kinachokujia kila siku ya jumatatu hadi alhamisi.
Tuzo hizo zinazoendelea kwa sasa zinaandaliwa na shirika la kiislamu la kutetea haki za kiraia- MUHURI.

>>Editorial desk