HabariNews

Wahudumu wa bodaboda kaunti ya Mombasa watishia kufanya maandamano.

Wahudumu wa bodaboda kaunti ya Mombasa wametishia kufanya maandamano kufuatia hatua ya rais Uhuru Kenyatta kutoa agizo la kuwataka kusajili upya pikipiki zao.
Wanaseme hatua ya rais Kenyatta kufutilia mbali usajili huo haifai kuathiri wahudumu wa pikipiki Kenya nzima.
Wanasema tukio hilo lilitendeka jijini Nairobi hivyo wahudumu wa pikipiki jijini humo wanafaa kuwajibishwa pekeyao.
Haya yanajiri siku chache baada ya wahudumu wa bodaboda kaunti ya Nairobi kunaswa kwenye video wakimnyanyasa kimapenzi mwanamke mmoja baada ya kudaiwa kusababisha ajali.
Kufikia sasa Zaidi ya wahudumu 200 wa pikipiki wamekamatwa.