AfyaHabariLifestyleNewsSiasa

Afisa mmoja wa polisi anayetoa ulinzi kwa rais ameripotiwa kujiua kwa nyumbani kwake.

Afisa mmoja wa polisi anayetoa ulinzi kwa rais katika kitengo cha naibu wa rais William Ruto,ameripotiwa kujiua kwa nyumbani kwake eneo la Juja katika kauntia ya Kiambu.
Inadaiwa kwamba afisa huyo kwa jina Samuel Ngati,alijua kwa kujipiga risasi kichwani jana asubuhi .
Afisa huyo alikuwa pekee nyumbani kwake katika kambi ya polisi ya GSU kitengo cha Rekee na haijabainika sababu za kujiua kwake.
Bastola aina ya Jeriko iliyokuwa na risasi kumi na tatu na bunduki nyengine aina ya Trevor sub-machine zilipatikanwa nyumbani kwa afisa huyo.
Inaarifiwa kwamba afisa huyo mwenye umri 35 alitengana na mkewe miakia miwili iliopita baada ya kujaliwa watoto wa wili.
Maafisa wa upelelezi DCI katika eneo la juja wanakichunguza kisa hicho ili kubaini sababu za kujiua kwa afisa huyo.