HabariMombasaNewsSiasa

Chama cha ODM eneo la Rabai Kaunti ya Kilifi kuteuwa mgombea ubunge atakayejaza nafasi iliyoachwa wazi na Mbunge William Kamoti.

Chama cha ODM eneo la Rabai Kaunti ya Kilifi Kinahadi leo kuteuwa mgombea ubunge eneo hilo atakayejaza nafasi iliyoachwa wazi baada ya Mbunge William Kamoti kufariki dunia usiku wa kuamkia jana alipohusika kwenye ajali mbaya ya barabarani.
Kinara wa Chama hicho Raila Odinga hapo jana akiwa katika mazishi ya Kamoti aliesema ODM itateuwa mgombea mwengine ili aidhinishwe na tume ya uchaguzi IEBC katika zoezi linaloendelea la kuidhinisha wagombea viti vya siasa.
Kamoti alizikwa jana nyumbani kwake eneo la Kaliang’ombe-Rabai ana alifariki alipokuwa ametoka kuidhinishwa na tume ya uchaguzi IEBC ili kupigania wadhifa wake wa ubunge kwa muhula mwengine wa tatu.