HabariSiasa

WAGOMBEA WATANO WA UBUNGE WA KILIFI KASKAZINI WAIDHINISHWA NA IEBC

Tume huru ya kusimamia uchaguzi na mipaka nchini-IEBC imewaidhinisha wagombea watano wa kiti cha ubunge wa Kilifi kaskazini, hii ikiwa ni kutokana na wagombea wawili kufeli kufika mbele ya tume hiyo.
Kulingana na msimamizi wa tume hiyo eneo bunge la Kilifi kaskazini Hamisi Tsumo ni kuwa kati ya wagombea watano waliojitokeza mmoja ni mwanamke kutoka kwa chama cha Umoja Summit.
Hata hivyo ameeleza kuwa wagombea hao wawili waliofeli kufika mbele ya tume ya IEBC wamejiondoa rasmi kwenye kivumbi hicho cha kuwania ubunge wa Kilifi kaskazini haya yakithibitishwa na vyama vyao vya kisiasa.
Wagombea hao wawili wa kike ni wagombea wa chama cha Jubilee na kile cha Community Party Of Kenya.

>> News Desk.