HabariSiasa

Chama cha mawakili wa kike FIDA kuandaa kikao na wagombea mbali mbali wa urais Pamoja na wagombea wenza mwezi ujao.

Chama cha mawakili wa kike FIDA kitaanda kikao na wagombea mbali mbali wa urais Pamoja na wagombea wenza wiki ya kwanza ya mwezi ujao.
Kikao hicho kitaandaliwa katika ukumbi ambao utatangazwa baadaye.
Katika kikao hicho FIDA inalenga kufahamu jinsi wagombea hao watakavyoshughulikia maswala ya wananwake na Watoto kwa jumla iwapo watachaguliwa.
Miongoni mwa wagombea wa urais, William Ruto wa UDA ndiye mgombea pekee ambaye mgombea mwenza ni wa kiume akiwa ni Rigathi Gachagua.
Raila Odinga Wa Azimio yuko na Martha Karua, George Wajakoya wa The Roots party akiwa na Jostina Wagui na David Mwaure wa chama cha Agano akiwa na Ruth Mucheru.

>> News Desk…