Habari

Afisa mkuu mtendaji wa EACC amewataka viongozi wa kidini kuunga mkono taasisi za serikali.

Afisa mkuu mtendaji wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC Twalib Mbarak amewataka viongozi wa kidini kuunga mkono taasisi za serikali hususan tume huru ya uchaguzi nchini IEBC na tume ya EACC. Twalib akizungumza katika kongamano ambalo limewaleta pamoja viongozi hao wa kidini na maafisa wa EACC, Mbarak amesema kuwa kuna baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaodhalilisha taasisi za serikali baada ya wao kutoidhinishwa kuwania nyadfa mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa Agosti 9. Twalib amewataka viongozi wa kidini kuhamasisha umma kuhusiana na maadili na umuhimu wa kupiga kura vile vile kuwachagua viongozi wenye maadili.

>> News Desk…