HabariNewsSiasa

“Watumishi wa umma watapokea nyongeza ya mshahara” asema Aisha Jumwa.

Waziri wa utumishi wa Umma na Jinsia Aisha Jumwa ametangaza kuwa watumishi wa umma watapokea nyongeza ya mshahara kwa muda wa siku mia zijazo.

Akizungumza wakati wa kuzuru kituo cha huduma jijini Nairobi, Jumwa amebainisha kuwa serikali imetoa mabadiliko kadhaa ili kuboresha utoaji wa huduma kote nchini.

Aidha katika hatua ya kuboresha utoaji wa huduma katika kaunti zote 47, Jumwa amesema kuwa wizara itapitia masaa ya kazi ya vituo vyote 52 na pia kutaanzishwa vituo vingine zaidi.

Hata hivyo Katibu Mkuu wa utumishi wa umma Mary Kimonye, ametoa wasiwasi kuhusu vitambulisho ambavyo havijachukuliwa na kuwataka wakenya wajitokeze kwa wingi katika kituo ili waweze kuchukua stakabadhi zao.

BY EDITORIAL TEAM