HabariNews

NEMA yawaonya wachimba migodi wanaoendeleza shughuli hizo katika maeneo yaliyopigwa marufuku.

Halmashauri ya Mazingira nchini Nema imetishia kuwachukulia hatua za kisheria wachimba migodi wanaoendeleza shughuli hizo katika maeneo yaliyopigwa marufuku.

Kulingana na mkurugenzi wa halmashauri hio kwale Godfrey wafula kaunti ya Kwale iko maeneo yaliyoidhinishwa kwa shughuli hizo za uchimbaji, hivyo kuwataka kufuata sheria.

Ameutaja uchimbaji wa mawe na mchanga bila kufuata utaratibu kuwa tishio kwa usalama wa wenyeji kwani mashimo huachwa bila kufanyiwa ukarabati.

BY EDITORIAL DESK