HabariNews

WALIMU 25 ENEO LA BONI KAUNTI YA LAMU WASAFIRISHWA KUTUMIA NDEGE YA JESHI.

Walimu 25 wanaofundisha katika shule za msingi eneo la Boni kaunti ya Lamu wamepelekwa katika maeneo yao ya kazi kwa kutumia ndege ya jeshi.

Walimu hao wanaofundisha katika shule za Mararani, Mangai, Milimani, Basuba na Kiangwe, walishidwa kufika shuleni kutokana na hali ngumu ya usafiri hivyo shule hizo kusalia kufungwa.

Mkurugenzi wa Tume ya kuwaajiri walimu TSC kaunti ya Lamu Riziki Daido amesema walimu wapatao 30 zaidi watapelekwa katika maeneo ya Boni, naye mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Lamu Joshua Kaga akiwahakikishia walimu kwamba maslahi yao yatatekelezwa.

Naibu kaunti Kamishena na ambaye pia ni kaimu kaunti Kamishena Charles Kitheka, amewahakikishia usalama walimu hao.

BY EDITORIAL DESK