HabariNews

JAMII YAHIMIZWA KUDUMISHA UTANGAMANO.

Uwiano na utangamano miongoni mwa jamii ni jambo ambalo limekuwa likipewa upata kuona kuwa amani na umoja unadumishwa sawia na kukabiliana na visa mbalimbali vya utovu wa usalama.

Katika kikao eneo la Dzombo kaunti ya Kwale, afisa wa kitengo cha uwiano na utangamano katika shirika la Haki Yetu, Julius Wanyama, ametoa wito kwa jamii za Pwani kudumisha umoja pamoja na kutumia mbinu mbadala za kutatua mizozo ya kijamii ili kukabiliana na visa vya mauaji ya wazee.

Kadhalika wenyeji eneo hilo wameeleza baadhi ya masuala yanayochangia visa hivyo kuongezeka, kwenye Kikao hicho ambacho kimewaleta pamoja Mwakilishi wa serikali ya Kaunti katika wadi ya Dzombo, chifu wa eneo hilo pamoja na wazee wa vijiji.

Aidha idara ya usalama imeeleza baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo eneo hilo katika kutekeleza majukumu yao ikiwa ni ukosefu wa gari katika kituo cha polisi cha Mamba pamoja na ukosefu barabara nzuri.

BY JOYCE KELLY