HabariNews

Spika Mwambire na Wakazi Ganze walilia hofu ya ndovu Mashambani, Kilifi

Kuwa wakazi wa eneobunge la Ganze wamekosa imani na serikali kwa sababu ya ulegevu wa kushughulikia swala la ndovu wanaovamia mashamba na kuharibu mazao yao.

Ndovu hao kutoka mbuga ya wanyamapori ya Tsavo Mashariki wanaaminiwa kupiga kambi katika kijiji cha Forodhoyo katika kata ya Mrima wa Ndege, wadi ya Sokoke kwa mara ya saba sasa.

Kulingana na SPIKA wa Bunge la Kaunti ya Kilifi Teddy Mwambire, ndovu walivamia shamba lake siku ya Jumanne Septemba 12, 2023  mwendo wa saa mbili na nusu usiku ambapo juhudi za familia yake pamoja na mfanyakazi wa shamba waliwafukuza hazikufua dafu, ndovu hao walirudi kesho yake saa tisa alasiri.

Mwambire aliilaumu serikali ya kitaifa kutokana kero la uvamizi wandovu mara kwa mara wanaoharibu mimea katika mashamba yao. Hili limechangia ukosefu wa chakula na hali ngumu ya kukimu mahitaji ya wakuliima na wakaazi kwa jumla katika eneo bunge hilo.

“Serikali inaharibu tegemeo letu uchumi la uchumi. Tumepoteza imani na serikali ya kitaifa na maafisa wanaodai kuwa inashughulikia kero ya uvamizi wa ndovu,” akasema.

Spika alidokeza kuwa licha ya kutuma ombi katika bunge la seneti mnamo Julai kutaka serikali ya kitaifa kutenga pesa za kuzungusha ua la umeme katika mbuga ya wanyamapori ya Tsavo katika kaunti za Kwale, Taita Taveta, Kilifi na Tana River ili kuwazuia ndovu kuvamia makazi ya binadamu, hakuna majibu aliyopata huku wananchi wakiendelea kuteseka na kuhangaishwa na ndovu.

“Hakuna chochote kinachoendelea kutoka kwa serikali kudhibiti ndovu. Hata niliamua sitapiga ripoti kwa Shirika la Huduma kwa Wanyapori nchini (KWS) kuhusu uharibufu uliofanyika,” akasema.

Wakazi wa Ganze aidha walieleza hofu yao  kuendelea kuteseka na njaa kufuatia uharibifu mkubwa uliosababishwa na ndovu. Walilalamikia  uharibifu wa ekari za ya mahindi shambani, kuangushwa kwa migomba ya ndizi pamoja na mipapai.

Wakazi hao walielezea wasiwasi wao wakiachwa njia panda iwapo watalima wakati wa msimu wa mvua kuanzia Oktoba, Novemba na Desemba 2023 ama wataketi majumbani kusubiri chakula cha msaada kutoka kwa serikali na wahisani.

Mwambire hata hivyo aliwataka wakulima kutokufa moyo licha ya changamoto ya ndovu akiwasihi  kuendelea kukuza mazao kwenye mashamba yao.

“Nawahurumia wakulima wanaojituma lakini wanaoishia kupoteza mazao yote. Huku kwetu akina babu na akina nyanya walikuwa wanajitia moyo na msemo unaosema kuwa ‘mkulima hafi moyo’. Binafsi nimejipata katika hali hiyo baada ya shamba langu kuvamiwa kila mara na ndovu,” akasema.

Kwa upande mwingine shirika la uhiadhi wa wanyama pori nchini KWS ikijitete kuwe iliweka maafisa wake katika eneo la Vitengeni kuwafukuza ndovu walio katika wadi ya Sokoke na kuwarudisha porini.

BY EDITORAL DESK