HabariNews

Afueni! Mahakama Kuu Yasitisha utekelezwaji wa Hazina ya Uangalizi ya Seneti

Mahakama Kuu imesimamisha utekelezwaji wa Hazina ya uangalizi ya Seneti kufuatia kesi iliyowasilishwa na maseneta 6 wateule.

Maseneta hao sita wateule Miraj Abdillahi, Raphael Mwinzago, Catherine Mumma, Tabitha Munene, Hamida Kibwana na Crystal Asinge waliwasilisha kesi wakikashifu na kupinga Tume ya Huduma za Bunge (PSC) kwa kukosa kuwajumuisha kwenye hazina hiyo.

Sita hao waliwasilisha kesi ya kupinga utekelezwaji wa hazina hiyo wakidai kuwa uamuzi wa Tume hiyo ni wa kibaguzi huku wakihoji kuwa maseneta wana mamlaka ya kusimamia maswala ya kaunti.

“Katiba haitofautishi kati ya maseneta waliochaguliwa na walioteuliwa katika kutekeleza majukumu yao,” zilisomeka nyaraka hizo.

Aidha Mahakama imeagiza sita hao kuwasilisha ombi la kesi yao hiyo kwa Tume hiyo ya PSC ndani ya siku saba na majibu ya kuhusiana na kesi au ombi lao hilo kutolewa ndani ya siku hizo.

Kesi hiyo itatajwa Oktoba 12  mwaka huu ili kutoa maelezo zaidi.

BY EDITORIAL DESK