HabariLifestyleNews

Mafuta Yashuka bei kwa Shilingi 1, EPRA yatangaza bei mpya

Mamlaka ya Kudhibiti Kawi na Mafuta ya Petroli nchini EPRA imepunguza bei za mafuta kwa shilingi moja.

EPRA imetangaza kuwa Mafuta ya Petroli yamepungua bei kwa shilingi 1, mafuta ya Dizeli yakipungua kwa shilingi 1.20 nayo mafuta ya taa kwa shilingi 1.30.

Katika taarifa iliyotumwa katika Vyumba vya habari Jumanne  Jioni Mei 14, EPRA ilibaini kuwa bei hizo mpya zitaanza kutekelezwa kuanzia Mei 15 hadi Juni 14, 2024.

Punguzo hili la sasa linaashiria kuwa mafuta ya Petroli Mjini Mombasa yatauzwa kwa shilingi 189.66, Dizeli shilingi 176.01 nayo mafuta ya taa yakiuzwa kwa shilingi 165.69 kwa lita.

Jijini Nairobi lita moja ya mafuta ya Super petrol yatauzwa kwa shilingi 192.84, Dizeli 179.18 na mafuta ya taa kwa shilingi 168.76.

BY MJOMBA RASHID