HabariNews

Lazima Vitambulisho Mupewe, Odinga Akosoa Serikali na Gharama ya Stakabadhi Muhimu

Muungano wa Azimio La Umoja litatoa msimamo wake siku ya Alkhamisi kuhusiana na ripoti ya mazungumzo wa pande mbili.

Haya ni kwa mujibu wa Kinara wa Azimio Raila Odinga anayekashifu vikali Serikali kwa kukosa kuafikia ahadi zake kwa wananchi hasa wale wa kipato cha chini akitaja mikopo ambayo Serikali inaendelea kukopa inawaumiza wananchi.

Odinga aliitaka Serikali kufutilia mbali ada mpya zinazopendekezwa na Serikali katika utoaji wa Stakabadhi muhimu ikiwemo vitambulisho huku akiongeza kwamba Serikali inafaa kutoa vitambulisho hivyo bure kwa Wakenya.

Kulingana na kinara huyo, hatua hiyo itakiuka haki za vijana wengi ambao wanalilia ukosefu wa vitambulisho na kwamba kuna haja Serikali kushughulikia suala hilo.

Kitu ingine ambayo nitataka serikali hii ifanye ni kupeana kwa vijana vitambulisho, mupewe bila malipo maana kuna vijana wengi sana wametimu miaka kumi na nane na hawana vitambulisho. Vitambulisho ni haki ya kila mkenya sababu hio ni thibitisho ya kwamba wewe ni Mkenya.” Alesema

Haya yanajiri wiki chache tu baada ya Waziri wa Usalama wa ndani Prof. Kithure Kindiki kutangaza kupitia wa gazeti rasmi la Serikali ada mpya kwa stakabadhi hizo muhimu.

BY NEWS DESK