HabariNews

Zazaa la El-nino, Mashirika Yakipaza sauti wakaazi Kujilinda

Shirika la afya duniani WHO pamoja na taasisi ya utafiti wa kimatibabu nchini KEMRI yamewataka wananchini kuwa makini wakati huu wa mvua za elnino ili kujiepusha na ugonjwa wa Malaria.

Kulingana na Mashirika hayo huenda visa vya Malaria na magonjwa mengine vikaripotiwa kufuatia mvua inayoendeleaa kunya sehemu mbali mbali nchini hivyo kuwashauri wakaazi wa maeneo yaliyoathirika zaidi na mafuriko kuweka mikakati ya kujilinda.

Kwa upande wake shirika la Msalaba mwekundu nchini lilisistiza haja ya wananchi walioathiriwa na mafuriko kutotoka sehemu salama walizohamia mpaka viwango vya mvua vitakapopungua.

Micheal Ayabei ni afisa mkuu wa idara ya kukabili majanga katika shirika la msalaba mwekundu .

Ule ujumbe ningependa kuufikisha kwa wakaazi ni kwamba iwapo wameokolewa, hatakama wameona viwango vya maji vimeshuka wasirudi katika makaazi hayo mpaka kuwe salama kwasababu tumepata visa amabo watu amabo waliokolewa wiki mbili zilizopita walirudi katika mashamba yao na ikatubidi kuwarudia sababu hatuwezi kukubali kupoteza maisha” Alisisitiza

Haya yanajiri huku shirika la utabiriwa hali ya anga nchini likitoa bishara ya kuendelea kwa kushuhudiwa kwa mvua maeneo ya kusini mwa kenya huku pwani kukitabiriwa joto la zaidi ya nyuzi 30.

BY NEWS DESK