HabariNews

Mvua ya Maafa Voi yazua Zaizai Wakazi zaidi ya 500 wakiaathirika

Mwili wa mwanamume mmoja umepatikana katika mtaa wa Railway mjini Voi baada ya kushudiwa mvua kubwa eneo hili inayoenedelea kunya maeneo mbali mbali humu nchini.

Mwili huo ulipatikana ukiwa umejaa matope na kuelee kwenye maji yaliosababishwa na mafuriko yaliotokana na mvua kali.

Mvua hiyo inakadiriwa kuathiri watu zaidi ya 500 katika eneo hilo huku wengine wakiachwa bila makao.

Mwili huo hata hivyo unaendelea kuhifadhiwa katika Hospitali ya Rufa ya Moi mjini Voi huku maafisa wa kutoka shirika la msalaba mwekundu wakiendelea na zoezi la kutambua familia mbalimbali ambazo zimeathirika na mvua hiyo.

BY NEWS DESK