HabariKimataifaLifestyleMombasaNews

Baadhi ya Waumini Waanza Mfungo; Wito Ukitolewa Kuzingatia Utukufu wa Mwezi wa Ramadhan

Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu nchini na kote ulimwenguni wameanza ibada ya mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan hii leo.

Waumini hao wametekeleza ibada ya funga ambayo ni nguzo ya 4 katika nguzo 5 za dini ya Kiislamu, huku ushauri na wito ukitolewa kwa waumini kusaidiana na kuepuka migogoro ya kidini sawia na ksuaidiana hasa katika kipindi hiki kigumu cha kiuchumi.

Wakiongozwa na Sheikh Abubakar Bini, Mwenyekiti wa baraza la Maimamu na wahubiri CIPK, katika eneo la kaskazini mwa bonde la ufa, viongozi hao wamehimiza wafanyabiashara wa kuuza bidhaa za tende na nyingine nyingi kwa bei nafuu kwa waumini na kukoma kupandisha bei.

“Tunashukuru Serikali kwa kuondo ushuru wa tende na hiyo ni mujimu sana, sasa basi tunahimiza wafanyabiashara nao wasipandishe bei na kumuumiza mwananchi kwa msimu huu.Alisema Sheikh Bini.

Viongozi aidha waliipongeza Serikali kwa kuondoa ushuru wa bidhaa za tende ambayo ni bidhaa muhimu kwa waislamu wakati wa mwezi huu mtukufu.

Aidha walitoa wito kwa waislamu wote kufuata kanuni za mwezi huu mtukufu ili kuombea hali ya kudorora kwa uchumi kote duniani pamoja na vita vinavyoshuhudiwa katika mataifa tofauti tofauti duniani ikiwemo Sudan na huko Ukanda wa Gaza nchini Palestine.

 

BY NEWSDESK