HabariNews

Siku ya wanawake ulimwenguni

Huku Kenya ikiungana na mataifa mengine ulimwenguni kuadhimisha siku ya wanawake leo, idara ya jinsia kwale imetaja utumizi mbaya wa mitandao umechangia pakubwa mauwaji ya wanawake nchini.

Akizungumza katika sherehe hiyo afisaa wa idara hiyo Nelly Amoite amekashifu vikali mauwaji hayo ambayo yamekuwa yakiripotiwa katika siku za hivi karibuni kote nchini, wito umetolewa kwa jamii kukomesha visa vya mauaji ya wanawake duniani.

Kwa upande afisa wa shirika la kijamii la Samba Sports Youth Agenda Mwanaisha Kuwania ameitaka jamii kutonyamazia suala hilo na badala yake kuanzisha mazungumzo ya kupinga utekelezaji wa visa hivyo.

Haya yanajiri huku hafla ya kusherekea siku ya wanawake duniani imeweza kufanyika katika uwanja wa maonyesho wa Ukunda eneo bunge la Msambweni.

BY NEWS DESK