HabariNews

Naibu gavana wa Kisii Dr Robert Monda ni Fisadi,Maseneta wamuondoa Ofisini.

Gavana wa Kisii Simba Arati sasa ana muda wa siku kumi na nne kumteua naibu gavana mwingine baada ya bunge la Seneti kumuondoa ofisini naibu wake  Dr Robert Monda baada ya naibu gavana huyo kupatikana na hatia  katika makosa yote manne yaliyowasilishwa mbele  ya maseneta wa Bunge hilo.

Katika kura zilizopiwa Karibu saa sita usiku na maseneta 43 waliokuwa bungeni wakati wa Kupiga kura ili kuamua hatima ya naibu gavana huyo, zaidi ya maseneta 24 waliunga mkono makosa yote manne dhidi yake, makosa yaliyojumuisha ukiukaji wa katiba, Matumizi mabaya ya Ofisi, ukiukaji wa Madili pamoja na uhalifu dhidi ya sheria za kitaifa.

Katika kosa la kwanza la ukiukaji wa katiba,maseneta 39 waliunga mkono kubanduliwa kwake, maseneta 3  wakapinga huku mmoja akisusia kupiga kura.

Idadi sawia na hiyo ilipiga kura katika kosa la pili la matumizi mabaya ya Ofisi ambapo maseneta 3 walipinga kubanduliwa kwa naibu huyo wa gavana, 39 wakaunga mkono kubanduliwa kwake huku seneta mmoja  akidinda kupiga kura.

Katika Kosa la tatu la ukiukaji wa madili, maseneta 35 waliunga mkono Robert Monda abanduliwe ofisini, maseneta 7 wakapinga kung’atuliwa kwake huku seneta mmoja akikataa kupiga kura yake.

Katika kosa la nne na la mwisho uhalifu dhidi ya sheria za kitaifa ambapo maseneta 32 waliunga mkono, maseneta 10 wakapinga huku seneta mmoja akikataa kupiga kura.

Daktari Robert Monda ameng’atuliwa ofisini  baada ya maseneta zaidi 24 kuunga mkono kila Kosa dhidi yake  kwa misingi ya ushahidi uliowasilishwa mbele yao.

“Waheshimiwa maseneta, matokeo ya upigaji kura yanaashiria kuwa bunge la seneti limeunga  mashtaka yafutayao ya mchakato wa kubandua ofisini naibu gavana wa kaunti ya kisii DR Robert Monda. Shtaka la kwanza la ukiukaji wa katiba, Shtaka la pili la matumizi mabaya ya ofisi,Shtaka la tatu  la ukosefu wa madili na a shataka ya nne la  uhalifu dhidi ya sheria za kitaifa.”Alisema Spika Kingi.

Akizungumza katika Bunge hilo, seneta  wa Kakamega alielezea kusikitishwa kwake na kiwango cha ufujaji wa pesa za umma katika kaunti ya Kisii ambao uliendeshwa na naibu huyo wa gavana.

“Baada ya naibu gavana kupokea laki nane zinazodaiwa, kwa haraka alituma pesa hizo kwa Lucy kisha akamwambia pesa hizo ni za shughuli ambazo tulikuwa tumeongea. Kisha, Lucy akamwambia rejesha pesa hizo.Lucy akamrejeshea Pesa hizo. Hii ndio inaitwa uadilifu. Kufanya mambo yanayofaa hata wakati hakuna mtu anakuona.” Alisema Boni Khawale.

Aidha, maseneta hao walikerwa na mienendo na vitendo vya Robert Monda wakisema ni ukosefu mkubwa wa ki madili kwa kiongozi kuhusika na visa vya ufisadi akilenga kufaidi familia yake, watu wa aila yao au ata jamiii anayotoka.

“Bwana spika ,leo nimekasirika sana kuona baba akitoa ushahidi dhidi ya mwanawe, mtoto akitoa ushahidi dhidi ya babake, naye babake akitoa ushahidi dhidi ya mama wa kambo. Bwana spika, tabia gani hii tunakifunza kizazi cha sasa. Inasikitikisha na ni aibu kubwa.” Alifoka Ledama

 

Dr Robert Monda ameingia katika vitabu vya historia kama naibu gavana wa kwanza kubanduliwa ofisini tangu ujio wa ugatuzi

BY ISAIAH MUTHENGI