HabariNews

Serikali Yapumua; Mahakama Kuu Yakataa Kusitisha Utekelezwaji wa Sheria ya Nyumba za bei Nafuu

Mahakama Kuu imekataa kusitisha utekelezwaji wa Sheria ya Ushuru wa nyumba za gharama nafuu iliyotiwa saini na Rais William Ruto siku ya Jumanne.

Badala yake Jaji wa Mahakama hiyo Chacha Mwita ameagiza suala la maombi hayo lifikishe kwa pande zote mbili kwa haraka iwezekanavyo ndani ya muda wa siku 7.

Zaidi ya hayo mahakama hiyo imesema suala la kesi hiyo linaibua maswali muhimu ya msingi na yanayohitaji kusikilizwa kwa dharura.

Sasa Pande zote katika kesi hiyo zitaangazia masuala ya kesi hiyo Mei 16 mwaka huu.

Uamuzi huo unakuwa ushindi kwa serikali na sasa itatekeleza sheria hiyo hadi pale ksei hiyo itakaposikilizwa na kuamuliwa mustakbali wake Mwezi Mei.

Ikumbukwe kuwa Kesi hiyo iliwasilishwa na Wakenya watano wakidai Sheria hii ni njama ya serikali kutaka kufaidi watu wachache ambao watakuwa wakisimamia hazina ya nyumba.

BY MJOMBA RASHID