HabariNews

Serikali Yasitisha Usambazaji Wa Mihadarati Ukanda Wa Pwani

Serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha inasitisha usambazaji wa mihadarati na dawa za kulevya eneo la Pwani.

Kwenye mahojiano ya kipekee na meza yetu ya habari afisini mwake kamishna wa ukanda pwani Rhoda Onyancha amesema usambazaji wa dawa za kulevya umeenda chini eneo hilo akidokeza kuwa waraibu wameanza kutumia njia mbadala za kutumia dawa za madukani kutokana na uhaba wa dawa za kulevya.

Onyacha aidha amedokeza kuwa kumekuwa na ongezeo la idadi ya watu katika vituo mbali mbali vya kurekebisha tabia akisema kwamba hatua hiyo imeonyesha kuwa waraibu wanapata changamoto ya kupata dawa za kulevya na mihadarati.

“Tumeanza kuona matunda kwa sababu tumeona wengine wameanza kutumia dawa za duka kumanisha usambazaji wa mihadarati inaenda chini na wanajaribu kutumia njia mbadala,kwa hivyo tumejaribu sana na ukiangalia kwa hivyo vituo vyetu namba imeongezeka kumanisha mahali walikuwa wanapata hizi dawa zimeenda chini.” Alisema Onyancha.

Wakati huo huo Onyancha amewasishi washikadau pamoja na viongozi wa kijamii kushirikiana na jamii katika kufanikisha vita dhidhi ya mihadarati na kuhakikisha kwamba vijana ambao hawajaathirika hawaingizwi katika maswala haya.

“Tumeeleza maafisa wetu kwamba waweze kufanya mikutano vijijini mwao ambayo itahusisha washikadau wote ili kuwahusisha wazazi kuangalia mienendo ya watoto wao,na tunaomba washikadau wote washirikiane na sisi hasa viongozi ambao wanafaa kuwa mstari wa mbele kusiskizwa na jamii iliyomchagua.” Alisema Onyancha

BY MEDZA MDOE