HabariNews

Serikali Yaahidi Kushirikiana Kukabili Dhulma Za Kijinsia Pwani

Naibu msemaji wa serikali Mwanaisha Chidzuga ameihakikishia ofisi ya kamishna wa ukanda wa Pwani ushirikiano wa kikazi ili kukabiliana na dhulma za kijinsia miongoni wa watoto wakike na kiume ukanda huu.

Chidzuga akizungumza na meza yetu ya habari hapa Mombasa baada ya kufanya mkutano wa faragha na kamishna wa ukanda huu Rhoda Onyancha alieeleza kuwa afisi yake itashirikiana na afisi ya kamshina katika vita dhidhi ya dhulma miongoni mwa jamii za hapa Pwani.

“Tutashirikiana katika maswala ya kuwawezesha kina mama, ya mtoto wa kike,mihadarati,uhamasisho na usalama,tutashirikiana na ofisi ya kamshina wa Pwani ili kuhakikhisha tuhamasisha watu wetu kuhusu  masawala ya maendeleo mashinani kama moja ya agenda yetu” Alisema Chidzuga

Wakati Huo Huo chidzuga aliziomba idara mbali mbali zinazotoa hamasa kwa watoto wa kike kujumuisha wa kiume kwani wote wanaathirika kwa njia moja au nyingine kwenye dhulma za kijinsia kuhakikisha wanaelimishwa vilivyo kuhusiana na swala hilo.

Vile vile Chidzuga alitoa wito kwa watoto wa kike Pwani akiwataka kuzingatia masomo yao katika juhudi za kuhakikisha wanapata nyadhifa za juu serikalini na kutatua changamoto zinazosibu wakaazi wa Pwani.

“Maafisa wa usalama hawezi kutekeleza hayo yote akiwa pekeyake mimi nawasisihi viongozi wa Pwani hasa wa kisiasa,wanawake kwa wanaume,viongozi wa kidini watushike mkono maana tukishirikiana na tutaweza kusonga mbele na nimefurahishwa na uongozi wa kamshina huyu na tutazidi kumshika mkono” Aliongeza Chidzuga.

Ni kauli ambayo imepigwa jeki na kamishna wa kamshina huyo akionyesha haja ya ushirikiano kuwepo baina ya wazazi na asasasi mbali mbali za kiserikali na zisizo za kiserikali katika swala hilo pamoja na kuhakikisha swala la elimu linapewa kipaumbele Pwani.

“Tunajaribu kushirikisha wazazi na wengine ambao wanazungumzia jambo hilo ili kwa pamoja tuweze kuona mtoto wa kike yuko sawa,kuna jambo ambalo tunafanya kuhakikisha watoto wanenda shule” Alisema Onyancha

BY MEDZA MDOE