HabariNews

Kongamano la kitaifa la kina mama jijini Mombasa

Joyce Mwikali Mutinda amewahimiza kina mama kuwania nafasi za uongozi kama njia mojawapo ya kusawazisha thuluthi mbili ya kijinsia.

Akizungumza katika kongamano la kina mama lililoandaliwa hapa mjini Mombasa, Joyce Mwikali alisisitiza kuwa pana haja ya kukumbatia uongozi wa kina mama katika nyadhifa zote serikalini.

Aidha mwenyekiti huyo alisifia utawala wa Rais William Ruto kwa kuwa mstari wa mbele kukumbatia uongozi wa kina mama akiongeza sera za tume hiyo zitahakikisha thuluthi mbili za kijinsia imeafikiwa katika nyadhifa za uongozi.

”Kama Tume ya usawa na jinsia tunalenga kuwekeza pakubwa katika uongozi wa kina mama. Serikali kuu imelipa suala hili kipaumbele na leo tumeandaa kongamano hili ili kutoa mafunzo kwa kina mama kuhusu uongozi. Kina mama wakiwa viongozi itakuwa afueni sio tu kwao bali pia kwa serikali, kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.”Alisema Mwikali

Mwikali kadhalika aliwataka wabunge wote wa mabunge yote mawili ya kitaifa kuifanyia katiba marekebisho kwa kugeuza baadhi ya vipengee vya katiba ili kubuni sheria mpya zitazounga mkono mapendekezo yaliyowasilishwa na tume hiyo ili kuhakakisha usawa wa kijinsia umeafikiwa.

“Kuhusu suala la thuluthi mbili ya jinsia, itakuwa vema iwapo marekebisho ya katiba yatafanyiwa ibara ya katiba ili kuhakikisha vipengee husika vimefanyiwa marekebisho. Pia vyama vya kisiasa vina mchango mkubwa kufanikisha suala hili la kijinsia. Tunawahimiza wabunge wa mabunge yote mawili wapitishe mswada huu ili kufanikisha thuluthi mbili za jinsia.” Alisema Mwikali.

Mwenyekiti huyo aidha hakusita kukashifu vikali dhuluma za kijinsia zinazoshushudiwa nchini na kuitaka idara ya upelelezi wa jinai DCI pamoja ofisi ya kiongozi wa mashtaka ya umma kuwachukulia hatua kali za kisheria wanaotekeleza dhuluma hizo dhidi ya wanawake.

“ Kila mtu ana haki ya maisha. Hakuna mtu aliye na mamlaka ya kumua mwenzake.Haijalishi iwapo ni mwanaume au mwanamke. Tunatoa wito kwa idara ya makosa na upelelezi wa jinai DCI kukabiliana na wahalifu wanaowaua wasichana wetu. DCI iwachukulie hatua za kisheria maramoja wote wanaohusika .”Alisema Mwikali

Kwa upande mkurungezi mtendandaji Quresha Abdillahi alisisistiza kuwa idara yake imeweka mikakati madhubuti itakayoshinikiza utekelezwaji kikamilifu wa sheria ya thuluthi mbili za jinsia humu nchini.

Aidha abdullahi hakusita aliungana na viongozi wengine kusuta vikali  dhuluma na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake huku akitoa wito kwa  jamii kuungana pamoja kupinga dhuluma za sampuli hiyo.

“Si jukumu la mtu mmoja,ni jukumu la jamii nzima. Maafa haya yanafanyika mijini na vijijini. Sote tushirikiane na serikali kukabilian na janga hili ambalo linakua kwa kasi. Si jukumu la serikali tu,sote tuungane kulinda maisha ya wasichana na wanawake kwa jumla.” Alisema Abdullahi.

Kuandaliwa kwa kongamano hilo kulijiri siku chache tu baada ya shrehe ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani Machi tarehe 8. Kauli ya mbiu ya Kongamano la mwaka huu la kina mama ilikuwa ni kuwawezesha kina mama katika uongozi kupitia  malengo, uthabiti na usawa kwa wote.

BY ISAIAH MUTHENGI