BurudaniEntertainmentHabariLifestyleMombasaNewsVideos

Mfahamu Bozen Msanii Mchanga lakini Tishio kwa kina Simba na Tembo!

Ni msanii anayekuja kwa kasi sana kwenye Tasnia ya Mziki wa Bongo Flavour, sio kwa kipaji chake tu lakini kuanzia muonekano uandishi wa ngoma zake na jinsi anavyoweza kucheza na hisia za mashabiki wake. Bozen ni msanii ambaye kwa mara ya kwanza kabisa aliweza kuachia kazi zake “Fine” na “Tulizana” ngoma ambazo zilipokelewa na mashabiki nchini Tanzania nan je ya Tanzania ikiwemo Mombasa na sehemu nyingi za Pwani Ya Kenya. Bozen Pia ndo Msanii wa kwanza kuwahi kufananishwa na msanii Latinoh aliyekuwa chini ya Uongozi wa Nadia Mukami kwa jinsi anavyoimba na mashairi yake. Bozen ameahidi kuachilia ngoma baada ya ngoma baada ya msimu huu wa Ramadhan.

Hata hivyo Bozen Ni msanii ambaye endapo atapa nafasi basi huenda akaipeperusha bendera ya Tanzania na Africa Mashariki kwa ujumla. Kwa sasa yuko na Kazi mpya mahsusi kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Hizi baadhi ya kazi zake hapa.