HabariNews

Afueni kwa Wakenya; Kenya Power Yapunguza Bei ya Umeme kwa asilimia 13.7

Ni Afueni kwa Wakenya sasa watafurahia ada nafuu za gharama za umeme kufuatia kushuka kwa bei za umeme kwa mwezi huu wa Aprili.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu Aprili 15 na Shirika la umeme Kenya Power ilitangaza punguzo la asilimia 13.7% ya umeme kwa wateja wa nyumbani.

KPLC ilihusisha kushuka kwa ada za umeme ni kutokana na kuimarika kwa shilingi ya Kenya dhidi ya Dola na vile vile kushuka kwa bei za mafuta yanayotumiwa kuzalisha na kusambaza umeme.

Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa KPLC, mhandisi Dkt. Joseph Siror amesema punguzo la asilimia 37 la gharama za mafuta kati ya Machi na Aprili mwaka 2024 kama ilivyotangazwa na Mamlaka ya kudhibiti Kawi na Mafuta ya Petroli EPRA lilikuwa mojawapo ya mchango mkubwa katika kuopunguza bei za umeme.

“Tunafuraha kutambua kuwa kupunguka, kumetoa ahueni kwa wateja wetu na tuna matumani kuwa mazingira ya Uchumi mkuu na kuimarika kwa hali ya usambazaji wa huduma zetu zinazotumia mafuta, kwa hiyo tutaumia kawi kidogo yam aji na kurahisisha shughuli…” alisema Dkt. Siror, Mkurugenzi Mtendaji wa KPLC.

Kwa wateja wa kitengo cha 1 cha ushuru wa Wateja wa nyumbani (DC 1) wanaotumia chini ya uniti 30 kwa mwezi sasa watalipa shilingi 629 kwa mwezi wa Aprili mwaka huu kutoka shilingi 729 kwa uniti sawia mwezi uliopita, hili likiwa ni punguzo la asilimia 13.7.

Na kwa wateja walio chini ya kitengo cha 2 cha ushuru wa Mteja wa Nyumbani (DC 2) wanaotumia wastani wa uniti 31 hadi 100 kwa mwezi sasa watalipa shilingi 1,574 kutoka shilingi 1,773 ya mwezi Machi, ikiwa ni punguzo la asilimia 11.2.

Halkadhalika kwa wateja chini ya kitengo cha 3 cha ushuru wa Mteja wa Ndani/Nyumbani (DC 3) wanaolipia uniti zaidi ya 100 kwa mwezi watalipa shilingi 3,728 mwezi huu wa Aprili kutoka shilingi 4,127 mwezi Machi ikiwa ni punguzo la asilimia 9.7.

BY MJOMBA RASHID