HabariNews

Idara ya hali hewa yatahadharisha ujio wa mvua kubwa kupita kiwango nchini

Idara ya Utabiri ya hali Anga nchini, MET imetoa tahadhari ya mvua kubwa zitakazopita kiwango na kusababaisha mafuriko zaidi katika baadhi ya maeneo nchini.

Maeneo yanayotarajiwa kupata mvyua hizo ni pamoja na Magharibi mwa Kenya yakiwemo Kisumu, Siaya, Homa Bay, Busia, Migori na Kisii.

MET imesema pia maeneo ya Bonde la Ufa, Trans Nzoia, Uasin Gishu, Kirinyaga, Nyeri, Laikipia na Nairobi yatashuhudia mvua hizo.

Wakati uo huo kaunti zote 6 za ukanda wa pwani zikiwemo Mombasa, Kwale, Taita Taveta, Kilifi, Tana River na Lamu pia zitapa amvua hizo za kuongezeka.

Wakazi wa maeneo hayo yanayotajiwa kupata mvua hizo wakaonywa kuchukua tahadhari na kukoma kuvuka mito iliyofuriko au maeneo yaliyo na mafuriko sawia na kuhamia maeneo ya juu ili kuepuka majanga.

Haya yanajiri huku mvua kubwa ikianza kushuhudiwa kaunti ya Mombasa na viunga vyake mnamo siku ya Jumatatu.

BY NEWS DESK