HabariLifestyleNews

Wabunge Wanawake Washinikiza Waziri Nakhumicha Afutwe Kazi kwa Utepetevu

 

Wabunge wa kike sasa wanashinikiza kufutwa kazi kwa waziri wa afya Susan Nakhumicha kutoka na matatizo kulemaa ka shughuli za sekta ya afya nchini.

Wakiongozwa na Mbunge wa Githunguri Gathoni Wamuchomba na mwenzake wa Suba Kaskazini Millie Odhiambo wabunge hao wameeleza kukerwa na hatua ya kusitishwa kwa mpango wa Linda Mama uliokuwa ukisaidia kulipia ada za kujifungua hasa kwa akina mama wengi wanaotoka familia zisizojiweza.

Kulingana na wabunge hao kukatizwa kwa mpango huo kumepelekea shida kubwa na matatizo mengi huku wakihofia kuongezeka kwa idadi ya vifo vya watoto na akina mama waja wazito hasa huku mgomo wa madaktari ukiendelea.

Mwakilishi wa kike kaunti ya Kilifi Getrude Mbeyu mmoja wa kundi hilo na wabunge wanawake amesisitiza kufutwa kazi mara moja kwa Waziri Nakhumicha kwa kuwatia aibu akina mama.

Waziri Nakhumicha anatarajiwa kukumbana na wakati mgumu Jumatano Aprili 17 atakapofika mbele ya bunge kujibu maswali kuhusu mgomo wa madaktari unaoendelea huku tayari ikiwa mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino akiendelea kukusanya saini kabla kuwasilisha mswada bungeni wa kutokuwa na Imani na waziri huyo.

BY MJOMBA RASHID