HabariLifestyleNews

Walipeni Madaktari Pesa Wanazozihitaji! Rais Awashambulia Wanaounga Mkono Mgomo wa Madaktari,

Rais William Ruto amewasuta viongozi wanaounga mkono mgomo wa madaktari unaoendelea akiwataja kuwa wanaosaka umaarufu miongoni mwa Wakenya.

Akizungumza kwenye Kongamano la Kitaifa kuhusu gharama na Matumizi ya Serikali Kuu katika Ukumbi wa Bomas jijini Nairobi Rais amebaini kuwa viongozi wanaounga mkono mgomo wa madaktari kushinikiza matakwa yao wanapaswa kuwalipa madaktari mahitaji wanayoshinikiza.

“Ikiwa unaunga mkono mgomo basi lipa pesa wanaoziitisha madaktari. Lazima tukomeshe kutafuta umaarufu na badala yake tufuate lile ni sahihi,” rais alisema.

Rais aidha amesisitiza kuwa taifa lina matatizo makubwa zaidi ya kuyashughulikia kwa sasa hivyo akipuuzilia mbali lalama na matakwa ya madaktari.

“Tuna changamoto ya madaktari. Hatuwezi kuwalipa tumesema tua masuala na matatizo mengine makubwa tunataka kupambana nayo. Kisha tunapata tuna viongozi kama magavana wengine wanaunga mkono mgomo wa madaktari.” Alisema.

Kiongozi huyo wa taifa amewalaumu baadhi ya magavana wanaounga mkono mgomo huo akisisitiza kuwa viongozi wanapaswa kuwa mstari wa mbele kwa uongozi na kuacha alama ya uongozi kwa utendakazi bora badala kutafuta umaarufu wa kisiasa.

BY MJOMBA RASHID