AfyaHabariLifestyleMombasaNews

Kisa cha Kwanza cha Ugonjwa wa Mpox Chathibitishwa Taita Taveta

Wizara ya Afya imethibitisha kisa cha kwanza cha Ugonjwa wa Mpox unaojulikana kama Monkeypox katika mpaka wa kituo kimoja eneo la kaunti ya Taita Taveta.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Katibu Mkuu wa Afya ya Umma katika Wizara ya Afya Mary Muthoni amebainisha kuwa ingawa ni kisa kimoja tu cha ugonjwa huo kimerekodiwa, hiyo pekee inatosha kutangaza mlipuko wake.

Aidha Muthoni amesisitiza kuwa halaiki kubwa ya watu kati ya Kenya na nchi nyingine za Afrika Mashariki hasa kupitia njia za uchukuzi za Kaskazini na Kati inaleta hatari kubwa kwa kusambaza kisa hicho, ikizingatiwa kwamba nchi kadhaa katika kanda hiyo kwa sasa zimeripoti kesi hiyo.

Shirika la Afya Duniani WHO linasema kuwa ugonjwa wa Mpox ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vya monkeypox, ugonjwa ambao unaweza kusababisha upele mchungu.

Wakenya wametakiwa kufuata miongozo ya afya kama vile kunawa mikoni mara kwa mara na kuepuka kuwasiliana au kusogeleana kwa karibu na watu walioambukizwa.

BY NEWSDESK