HabariMombasaNews

Wanyakuzi wa Ardhi za Wavuvi Waanze Kuondoka; Waziri wa Madini na masuala ya Uvuvi

Serikali ya Kitaifa kupitia Wizara ya Madini, Uvuvi na Uchumi wa baharini imeapa kuwafurusha mabwenyenye walionyakua ardhi za kuegesha maboti ya wavuvi.

Serikali imewataka waondoke katika sehemu hizo mara moja kabla ya sheria kuchukua mkondo wake.

Akizungumza mjini Mombasa Waziri Hassan Ali Joho amesema wavuvi wamekuwa wakipitia changamoto kwa kukosa maeneo maalum ya kuegesha maboti yao wanapotoka katika shughuli za uvuvi.

“Kama umejenga mahali ambako ni kwa wavuvi anza kuhama polepole, wavuvi wetu wamekuwa wakiteseka sana. Kitu muhimu zaidi ni mtu akija na boti yake awe na mahali pa kuegesha na afikishe samaki wake aweze ku process na wafikie sokoni.” Alisema.

Joho amewahakikishia wavuvi hao kuwa serikali itatoa ilani muda mwafaka wa mabwenyenye hao kuondoka katika maeneo hayo za kuegesha maboti ya wavuvi.

Kuna takribani sehemu 46 za kuegesha maboti Mombasa na nyingine ziko Kilifi, baadhi ziko Kwale, Lamu, Tana River na hata Ziwa Viktoria; hizi tutafuatilia tuhakikishe zinarudi kwa wavuvi.” Alisema

Wakati uo huo Joho amebaini kuwa ujenzi wa kiwanda cha samaki eneo la Liwatoni kaunti ya Mombasa utakamilika katika kipindi cha muda wa mwaka mmoja ujao.

Amesema Serikali imempa mkandarasi mwengine jukumu hilo na hivi karibuni ujenzi huo uliokuwa umekwama kwa muda unatarajiwa kuendelezwa na kukamilika kwa wakati ili kuwanufaisha wakazi wa Pwani.

Tulikuwa na changamoto pale na sasa nataka kusema kuwa tumepata mkandarasi mpya, mikataba imetayarishwa na katika siku chache zijazo tutakuwa na mkandarasi sehemu hiyo na ujenzi utaanza rasmi na ndani ya miezi 8 hadi 12 ijayo tutaweza kufungua kiwanda hiki na kuanza rasmi kazi.

Na hakikisho ni iko raslmali nah ii ikamilika ajira zaidi zitapatikana hapa.” Alisema Joho.

 

By Mjomba Rashid