HabariMombasaNewsSiasa

Gavana Nassir aongoza Hafla ya Kuapishwa Wanachama wapya wa Bodi mbalimbali Mombasa

Gavana wa Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir ameongoza zoezi la kuapishwa kwa wenyekiti na wanachama walioteuliwa kusimamia Bodi mbali mbali katika serikali ya kaunti ya Mombasa.

Akizungumza katika hafla hiyo ofisini mwake gavana Nassir amesema kuwa uteuzi wa wajumbe hao unafungua ukurasa mpya katika dhamira ya kutoa huduma bora za maji na kuboresha utoaji wa huduma za afya Mombasa.

Nassir aidha amewapongeza wajumbe hao wapya na kuwataka wajitolee kutejeleza huduma bora kwa wakaazi wa kaunti ya Mombasa.

Niwapongeze wote hawa kwa kuteuliwa na leo kuapishwa kuchukua nafasi hizi. Tunahimiza hawa maafisa wasome na kuelewa manifesto yetu ili waitekeleze, hasa tukamilishe miradi ya miundominu na mifumo ya majitaka, maji safi na uhifadhi wa maji kutumika kule kwenye shida ya maji.

Pia suala la ujenzi wa sehemu ya wadi za kibinafsi katika hopsitali Kuu ya Pwani iendelezwe mazungumzo yamekuwa yakiendelea na tutafanikisha.” Alisema.

Wa kwanza kuapishwa Selina Maitha ambaye aliteuliwa na kuapishwa kuwa mwenyekiti wa bodi ya Kampuni ya usambazaji Maji Mombasa MOWASCO.

Naye Prof. Marleen Temmerman ameapishwa kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali Kuu ya Mafunzo na Rufaa ya Ukanda Pwani (Makadara) huku Khalid Omar akiapishwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya kufanya ithibati ya madeni katika serikali ya kaunti ya Mombasa.

By Mjomba Rashid