HabariNews

Waziri wa Barabara na Uchukuzi nchini Davis Chirchir amewaonya vikali wahandisi nchini dhidi ya utepetevu kazini

Waziri wa Barabara na Uchukuzi nchini Davis Chirchir amewaonya vikali wahandisi nchini dhidi ya utepetevu kazini na kuidhinisha ujenzi wa majumba na miundombinu duni ambayo inasababisha maafa na kuleta hasara.

Akizungumza katika ufunguzi wa kongamano la Kimataifa la 31 la  la Taasisi ya wahandisi , IEK, linaloandaliwa hapa mjini Mombasa, Waziri wa Barabara na Uchukuzi nchini Davis Chirchir alisema serikali imeweka mikakati na mipango maalum ya kukabili na pia kudhibiti mikasa inayotokana na kuporomoka kwa mnajengo nchini.

Waziri huyo kadhalika alisema serikali inashirikiana na wahandisi katika kufuatilia usajili wao na kuchukua tahadhari kwa kufuatilia kazi zao na miradi waliyopewa ya ujenzi wa majumba ili kuhakikisha usalama wa miundomsingi hiyo.

“Serikali imechukua hatua za kimaksudi kuwasajili wahandisi wote nchini ili Kufutailia kwa makini ujenzi wa majumba nchini. tunashirikiana na taasisi ya wahandisi kubaini wote wanaosimamia ujenzi wa majengo ili kuhakikisha wamefuata sera  na kutekeleza kazi yao kwa mujibu wa sheria.”alisema waziri Davis Chirchir.

Kwa upande Rais wa taasisi hiyo mhandisi Shammah Kiteme alisema utafiti wa Bodi ya waandisi nchini unaonyesha kuwa  kuna ukiukaji mkubwa wa taratibu zinazofaa kuzingatiwa ili kufanikisha ujenzi nchini kwa mujibu wa sheria hasa ikizingatiwa kuwa wengi wanaoendeleza ujenzi hawashirikishi wahandisi wenye tajriba na wataalam.

Akisema hali hii imechangia maafa makubwa na uharibifu wa mali isiyokadirika kutokana mapuuza ya sera na sheria zinazofaa kufuatwa kabla  ya kuidhinisha ujezni wowowte nchini.

“Utafiti uliofanywa na bodi ya wahandisi nchini unaonyesha kuwa  ni asilimia 14.7  wanaotumia mbinu zinazofaa na kufuata sheria zilizowekwa za ujenzi. Wawekezaji na wanakandarasi wanafaa kujua bila kuwahusisha wahandisi waliohitimu kunachangia kuporomoka kwa majengo. Hali hii pia imeleta hasara kubwa na kusababisha maafa.” Alisema Shammah

Shammah alitaka serikali ya kitafa  na pia serikali ya kaunti  kufuatilia kwa kina shughuli za ujenzi nchini ili kuhakikisha kuwa wahandisi wanaotwikwa majukumu ya kusimamia baadhi ya kandarasi wamehitimu kutekeleza shughuli hiyo.

“Kwa hivyo tunasema lazima kila mmoja afuate sheria zilizoko kwa kuwahusisha wataalam katika shughuli za ujenzi. Hii ni hakikisho kuwa ujenzi wao umeafiki vigezo na sheria za ujenzi ili kupunguza mikasa ya mara kwa mara.” Alisema Shammah

Kauli ya wawili hao inajiri huku visa vya majengo kuporomoka  nchini vikiripotiwa hali ambayo imesababisha maaafa na uharibifu wa mali isyokadirika nchini.

BY ISAIAH MUTHENGI