Serikali imehimizwa kujumuisha wakazi pamoja na mashirika ya kijamii katika kuendeleza kampeni za kitaifa ikiwemo shughuli ya upanzi wa miti iliyofanyika kote nchini.
Viongozi wamesema kuwa hatua hiyo itasaidia kutotumika vibaya kwa fedha za umma sawia na kupunguza gharama za safari na wajumbe wanaoandamana nao.
Kulingana na Mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya, kujumuisha jamii pamoja na mashirika ya kijamii ni mbinu inayofaa kutumiwa na serikali ili kupunguza matumizi ya fedha za umma kwenye shughuli zinazohusu taifa.
Baya alikashifu hatua ya viongozi wa serikali kusafiri sehemu tofauti tofauti kutumia usafiri wa ndege na misafara mikubwa ya magari, katika kuongoza shughuli ya upanzi wa miti ilhali shughuli hiyo ingesimamiwa na mashirika pamoja na jamii.
..
Kauli ya mbunge huyu inajiri baada ya mashirika ya kijamii kuikosoa serikali kwa kuwatuma mawaziri, makatibu na wakuu wengine serikalini katika sehemu tofauti humu nchini kuongoza upanzi wa miti. Prof Fred Ogola ni ofisa wa shirika la linda katiba.
..
Serikali kwa upande wake, ilishikilia kuwa miradi hiyo haikugharimu fedha yoyote kwani fedha zilizotumiwa zilitengwa kwa bajeti ya mwaka wa 2023/2024 na kushikilia kuwa hakuna fedha yoyote iliotumiwa vibaya Kimani Ichungwa ni kiongozi wa walio wengi katika bunge la Kitaifa.
..
Ikumbukwe serikali inapania kupanda miche milioni 500 kabla ya msimu wa mvua kuisha huku ikitarajia kupanda miti bilioni 15 kufikia mwaka wa 2032