Makala

Pesa za Vijana Mombasa County

Serikali ya kaunti ya Mombasa inasema imetenga shilingi milioni 1 kusaidia vijana zaidi ya 7000 kufungua  biashara zao.

Pesa hizo pia zitasaidia vijana ambao biashara zao zilisambaratika kuziinua upya.

Afisa mkuu wa maswala ya vijana kaunti ya Mombasa Inncocent Mugabe anasema pesa hizo ambazo hazina riba zitafaidi vijana wanawake pamoja na wale wanaoishi na ulemavi.

Mgabe anasema hatua hii ni katika juhudi ya kuinua vijana ambao asilimia Kubwa wameathirika kutokana na janga la Corona.

Seneta wa kaunti ya Taita Taveta Johnes Mwaruma ametoa wito kwa serikali ya kaunti hiyo kufanya mazungumzo na wahudumu wa afya wanaogoma badala ya kuwatisha kuwafuta kazi.

Mwaruma anasema wafanyikazi wana haki ya kushirikia mgomo na sharti serikali ya kaunti itafute mbinu ya kusuluhisha mgomo ambao umedumu zaidi ya mwezi mmoja sasa.

Haya yanajiri huku huduma katika hospitali zote za umma kaunti hiyo zikiendelea kuathirika na mgomo huo na juhudi za bunge la kaunti hiyo kutafuta mwafaka zikiambulia patupu.

Comment here