Baadhi wa viongozi wa siasa kaunti ya Tana River wanataka Bunge la kaunti hiyo kubuni sheria ambazo zitatumika kutoa miongozo kuhusiana na maswala ya malisho ya mifugo kaunti hiyo.
Kulingana na mwakilishi wa kike kaunti hiyo Bi Rehema Hassan amesema iwapo sheria hiyo itabuniwa itasaidia kupunguza mizozo wa mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji kaunti ya Tana River.
Hassan ameitaka idara ya usalama pamoja na ile ya mifugo kaunti hiyo kuhakikisha zinatekeleza sheria inayodhibiti uhamisho wa mifugo kutoka eneo moja hadi jingine.
Rehema,amesema hatua hiyo ni mojawapo ya kuepuka mizozo baina ya wakulima na wafugaji hususan ile ambayo imejitokeza eneo la Mwina kule Tana delta.
Comment here