Habari

Waathiriwa wa uchimbaji madini Kwale wahimizwa kujitokeza

Wakaazi walioathirika na shughuli za uchimbaji madini unaoendeshwa na kampuni ya Base Titanium kaunti ya Kwale wameshauriwa  kujitokeza katika vikao vya kutoa maoni.

 

Hii ni baada ya serikali kupitia wizara ya madini nchini kuzindua kamati ya maendeleo ya jamii (CDA) itakayohakikisha wakaazi hao wanafaidika na uchimbaji madini.

Wanachama wa kamati hiyo wakiongozwa na Mshenga Ruga wamesema kunaumuhimu wa walioathirika kujitokeza na kupendekeza miradi ya maendeleo wanayotaka.

Naye afisa wa jamii katika kampuni ya Base Titanium Pius Kassim amesema kamati hiyo itasimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika jamii.

Kassim ameelezea kuwa miradi hiyo itatekelezwa kupitia mgao wa asilimia moja ya mapato ya kampuni hiyo.

Comment here