Habari

Maendeleo ya Jamii CDA kupitia Base Titanium

Afisa msaidizi katika wizara ya madini nchini engineer John Mosonik amezindua rasmi kamati ya maendeleo ya jamii CDA inayolenga kujenga uwiano bora kati ya kampuni na ya uchimbaji madini ya Base Titanium na jamii ya maeneo ya Lunga Lunga hadi Likoni.

Itakumbukwa kuwa CDA ilipitishwa katika sheria ya madini tangu mwaka 2016 japo hadi sasa kamati hiyo haikuwa imezinduliwa rasmi kutokana na maswala yanayoambatana na muongozo wa kuitekeleza kikamilifu.

Aidha Kampuni ya Base Titanium ilipaswa kutoa fedha ya asilimia 1 ya mapato yake kila mwaka kusimamia utekelezaji kamilifu wa kamati hiyo ikiwemo kuiwezesha kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo wanayotaka jamii kufanyiwa.

Kufuatia hayo Mosonik ametoa changamoto kwa kamati hiyo kuhakikisha inatumia fedha hizo kwa uwazi na ipasavyo ili kumfaidi mwananchi.

Mbunge wa Lunga Lunga Khatib Mwashetani ni miongoni mwa wanakamati wa CDA.

Comment here