Makala

Kituo cha kuwalinda watoto chazinduliwa huko Diani kaunti ya Kwale

Serikali ya kitaifa ikishirikiana na shirika la Plan International imezindua kituo cha kuwalinda watoto katika kituo cha polisi cha Diani huko Msambweni kaunti ya Kwale.

Afisa wa shirika hilo Charles Nyukuri amesema kituo hicho kitatoa hifadhi kwa watoto wanaopitia visa vya dhulma za kijinisia katika kaunti hiyo.

Nyukuri pia amesema watoto wanaohusishwa na visa vya ukiukaji wa sheria wanatarajiwa kuzuiliwa katika kituo hicho cha polisi kabla ya kufikishwa mahakamani.

Kwa upande wake afisa wa shirika la kijamii la Kesho Kenya Lenard Musembi amesema kwamba kituo hicho kitawahudumia takriban watoto saba.

Musembi ameelezea kuwa watoto hao wanatarajiwa kuzuiliwa kwa muda katika kituo hicho ili kulinda haki zao.

Comment here