Mwakilishi wa wadi ya shimo la tewa ambae pia ni naibu kiongozi wa wengi katika bunge la kaunti ya kilifi Sammy Ndago amesema kwamba kaunti ya kilifi bado haijafikiana kuunga mkono ripoti ya maridhiano ya BBI.
Akizungumza katika mahojiano ya kwenye kipindi cha sauti asubuhi hii leo Ndago amesema kwamba kufikia sasa viongozi wa kaunti wamepanga kukutana na wanati wa eneo hilo kuwaelimisha kuhusu ripoti hiyo kabla ya kuipitisha katika bunge hilo.
Kadhalika ndago amepongeza kauli ya rais uhuru Kenyatta ya kusema kwamba wawakilishi wadi waondolewe mikopo na badala yake wapewe ruzuku kama wanavyopewa wabunge.
Mswada wa ripoti hiyo ulitumwa katika kaunti zote 47 wiki jana baada ya tume ya uchaguzi na mipaka IEBC kuidhinisha sahihi zaidi ya milioni moja katika harakati za kufanyia marekebisho katiba.
Comment here