Habari

Polisi wamefanikiwa kutibua jaribio la shambulizi la kigaidi kaunti ya Wajir.

Polisi wamefanikiwa kutibua jaribio la shambulizi la kigaidi kutoka kundi la kigaidi la al-shabaab, kushambulia kambi ya polisi katika eneo la Khorof-Harar kaunti ya Wajir.

Wapiganaji wa kundi hilo wamefyatua risasi katika kamabi hiyo kabla ya kuzidiwa nguvu na maafisa wa polisi.
Wakaazi wanasema kumekuwa na ufyatulianaji wa risasi kati ya kundi hilo na polisi kabla ya washukiwa hao wa Al shabaab kutoroka .

Polisi Zaidi wametumwa katika eneo hilo ili kuzuia mashambulizi kutoka kwa wanachama wa Al shabaab .

Na: Joseph Jira

Comment here