Habari

SERIKALI YAHIMIZWA KUWAHAMISHA BAADHI YA POLISI KATIKA KITUO CHA POLISI BAMBA

Serikali imehimizwa kuwapa uhamisho baadhi ya maafisa wa polisi katika kituo cha polisi Bamba katika eneo bunge la Ganze, kwa madai kwamba wanawahangaisha wakaazi eneo hilo.

Wakiongozwa na Amosi Kahindi wanasema baadhi  ya maafisa hao  wamekuwa na tabia ya kumwaga pombe ya mnazi kutoka kwa wachuuzi wa kileo hicho pamoja na kuwatia mbaroni  wakaazi ifikapo saa mbili usiku na kuzungushwa hadi saa sita usiku na kukiuka makataa ya kutotoka nje .

Kwa upande wake naibu kamishina eneo la Bamba George Chege amewataka wakazi hao kushirikiana na maafisa wa polisi na kufuata sheria kikamilifi.

Mzozo wa maafisa wa polisi na wakazi wa eneo hilo umekuwa ukishudiwa kwa muda mrefu sasa.