Habari

ZAIDI YA FAMILIA 50 HUKO KIWANJANI, VOI ZAHOFIA KUFURUSHWA KUTOKA KWA ARDHI YAO

Zaidi ya familia 50 zinazoishi Makina Kiwanjani eneo bunge la Voi Kaunti ya Taita Taveta zimegubikwa na hofu ya kufurushwa Katika makaazi yao kufuatia mzozo wa ardhi unaoendelea eneo hilo.

Hofu ya kufurushwa kutoka kwa makaazi yao imejiri baada ya baadhi ya nyumba zao kubomolewa  mwishoni mwa juma lililopita licha ya kupewa hati miliki za ardhi mwaka wa 2013.

Kwa Sasa wenyeji hao wamewataka viongozi wa kaunti ya Taita Taveta  kuingilia kati suala hilo baada ya juhudi zao za kusaka haki kugonga Mwamba.

Utata wa ardhi ni tatizo sugu linaloendelea kuwakosesha usingizi  Wakaazi wa Kaunti ya Taita Taveta na mkoa wa Pwani kwa ujumla kwa miaka sasa bila suluhu mwafaka.