Siasa

Wanaharakati wasema huenda mchakato wa BBI usiwe na manufaa

Wanaharakati wanaopinga mpango wa BBI hapa Mombasa wanasema huenda mchakato wa BBI usiwe na manufaa kwa wakenya kama inavyotarajiwa wakidai wawakilishi wadi nchini walihongwa ili kupitisha ripoti hiyo.

Katibu mkuu wa chama cha United green Movement-UGM Hamisa Zaja, anasema huenda viongozi wengi ambao wamehusika kupitisha ripoti hiyo wakakosa kuchaguliwa tena katika uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza na Sauti ya Pwani FM Bi Zaja amesema wawakilishi wadi walikosa kuhamasisha vyema wananchi kuhusu kilichomo ndani ya ripoti kwa kuwa MCAs wenyenye huenda hawana ufahamu kuihusu.