HabariSiasa

Muungano wa Jamii ya Waluo hapa Mombasa umezindua rasmi ofisi itakayokuwa ikitoa hamasa kuhusu mapendekezo ya katiba kupitia BBI.

Ofisi hiyo imezinduliwa eneo la Mikindani na inanuiwa kuwapa ufahamu zaidi wananchi kabla kufanyika kura ya maoni.

Mwenyekiti wa kundi hilo Jackonia Obado amesema lengo lao ni kuhakikisha raia wanapata mahali pakupata taarifa zaidi kuhusu BBI iwapo wanatashwishi na kipengee fulani.

Naye mwanachama wa kundi hilo Mary Mumbe amesema itakuwa vyema kwa wakaazi wa kaunti ya Mombasa kuendelea kupokea taarifa zaidi kuhusu ripoti hiyo, hata baada ya kupitishwa na bunge la kaunti ya Mombasa kabla ya kura ya maamuzi mwezi juni.

Maswala muhimu yanayofanyika katika ofisi hiyo ni kuwapa wakaazi nakala za ripoti ya BBI.

Mwisho