Habari

Serikali inasema uhaba wa fedha ni tatizo kubwa linalosambaratisha zoezi la serikali la kulipaji fidia waathiriwa wa mizozo baina ya wanyamapori na binadamu.

Waziri msaidizi katika sekta ya utalii Joseph Boinnet amesema kuwa hali hiyo imechangiwa na viwango vikubwa vya madeni yanoyoikabili sekta hiyo.

Hata hivyo Boinnet amesema serikali inapanga mipango kabambe kuhakikisha waathiriwa hao wanalipwa.